Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amezipongeza Yanga SC, Simba SC na Singida Black Stars kwa matokeo mazuri waliyopata katika michezo yao ya mashindano ya CAF iliyochezwa ugenini.
Ibenge amesema amefuatilia michezo ya timu hizo na kufurahishwa na namna zilivyowakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
Katika michezo hiyo, Yanga SC ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Gaborone United, huku Simba SC ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mighty Wanderers.
Kwa upande wa Singida Black Stars, timu hiyo ilipata ushindi mkubwa wa mabao 7-1 dhidi ya Al Ghazala, matokeo yaliyoiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kuendelea kupata matokeo chanya kwenye mashindano ya CAF.
Akizungumza kuhusu matokeo hayo, Ibenge amesisitiza umuhimu wa mshikamano miongoni mwa timu za Tanzania zinaposhiriki mashindano ya kimataifa.
“Kwenye mashindano ya CAF tunapaswa kuwa wamoja,” amesema Ibenge.
Matokeo hayo yanaendelea kuonyesha ushindani wa timu za Tanzania katika mashindano ya CAF, huku mashabiki wakisubiri michezo inayofuata na hatua zitakazochukuliwa na kila timu kuelekea hatua za mbele za mashindano hayo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni