Barcelona, Hispania
Winga wa FC Barcelona, Lamine Yamal, ameongezwa kwenye kundi la manahodha wa timu hiyo baada ya kupigiwa kura na wachezaji wenzake ndani ya kikosi.
Uamuzi huo unamfanya Yamal kuwa miongoni mwa wachezaji watano wanaounda kundi la manahodha wa Barcelona, akijiunga na Raphinha, Pedri, Frenkie de Jong na Eric GarcÃa.
Yamal, ambaye bado ana umri wa miaka 19, sasa anakuwa sehemu ya uongozi wa kikosi cha Barcelona, hatua inayompa nafasi kubwa zaidi katika majukumu ya ndani ya timu.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, uteuzi huo umefanyika kufuatia mchakato wa upigaji kura wa ndani wa wachezaji wa Barcelona.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni