US Open pia ilithibitisha kuwa Travis Scott alikuwa miongoni mwa mastaa waliohudhuria siku ya pili ya mashindano hayo kwenye USTA Billie Jean King National Tennis Center.
Rapa maarufu wa Marekani, Travis Scott, alionekana akiwa kwenye sehemu ya jukwaa ya timu ya Carlos Alcaraz wakati nyota huyo wa tenisi alipokuwa akicheza mechi yake ya kwanza katika US Open 2026 mjini New York.Scott alionekana akimpa sapoti Alcaraz wakati wa mchezo dhidi ya Roman Safiullin, ambao Mhispania huyo alishinda kwa seti tatu mfululizo za 6–4, 6–4, 6–4 na kutinga hatua ya pili ya mashindano. Uwepo wa Travis Scott ulivutia pia kutokana na uhusiano wake wa kibiashara na Nike, huku Alcaraz akiwa amevalia vifaa vya Nike vilivyohusishwa na chapa ya Cactus Jack ya msanii huyo katika mchezo huo.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni