Breaking


Jumamosi, 26 Septemba 2026

WAFAMASIA MNH-MLOGANZILA WATAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI WA HOSPITALI KATIKA JAMII



Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Julieth Magandi amewataka wafamasia kuwa mabalozi wazuri wa taasisi kwa kuhakikisha wanatoa huduma bora, kwa weledi na kuzingatia maadili ya taaluma, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha imani na uaminifu wa wananchi kwa hospitali. 


Dkt. Magandi amesema hayo wakati akizungumza katika siku ya maadhimisho ya wafamasia duniani  yaliyofanyika MNH-Mloganzila yenye kaulimbiu “Empowering pharmacists for healthier futures” 


Amesisitiza kuwa wafamasia wana nafasi muhimu katika kuhakikisha wagonjwa wanapata dawa sahihi, kwa wakati na kwa maelekezo yanayostahili, hivyo wanapaswa kutumia kila fursa wanapokutana na wagonjwa kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa. 


Ameongeza kuwa utoaji wa huduma kwa lugha nzuri, usikivu na heshima kwa wagonjwa ni sehemu muhimu ya kumjengea mgonjwa uzoefu mzuri wa huduma na taswira chanya ya hospitali.


Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Famasi MNH-Mloganzila amewataka wafamasia kuendelea kushirikiana na wataalamu wengine wa afya katika kuboresha huduma, ikiwemo kuimarisha ufuatiliaji wa matumizi na madhara ya dawa pamoja na kutoa taarifa kwa wakati pale changamoto zinapobainika.



Hakuna maoni: