Breaking


Jumanne, 15 Septemba 2026

WIZARA YA AFYA NA IOM ZATATHMINI MATOKEO YA UTAMBUZI WA NJIA ZISIZO RASMI NA KUIMARISHA AFYA MIPAKANI

 


Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Wahmaji (IOM) linafanya tathmini ya pamoja ya matokeo ya zoezi la utambuzi wa njia zisizo rasmi lililofanyika katika Wilaya za Momba na Ileje, pamoja na kuimarisha usimamizi shirikishi na kuwajengea uwezo watumishi wa afya katika mipaka ya Tunduma na Isongole.

Zoezi hilo linalofanyika mkoani Songwe kuanzia tarehe 13 hadi 18 Septemba 2026, pia linahusisha kupokea jengo la muda la uchunguzi wa afya za wasafiri katika mpaka wa Isongole, ambapo hatua hiyo inalenga kuimarisha uwezo wa uchunguzi, utambuzi wa mapema na mwitikio wa haraka dhidi ya magonjwa ya mlipuko na matishio mengine ya afya ya jamii.

Ushirikiano huo unalenga kuimarisha afya mipakani kwa kuwezesha mamlaka kutambua maeneo hatarishi, kuimarisha ufuatiliaji na utoaji wa taarifa, pamoja na kuhakikisha hatua za kinga na mwitikio zinafika hadi maeneo ya mipaka isiyorasmi.


Hatua hizi ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuimarisha utayari wa kukabiliana na dharura za kiafya kuanzia ngazi ya jamii hadi mipakani, kwa kuzingatia kuwa magonjwa hayana mipaka na hivyo ushirikiano, ufuatiliaji na mwitikio wa mapema ni muhimu katika kulinda afya za wananchi.

Hakuna maoni: