Breaking


Ijumaa, 16 Oktoba 2026

BI, ANGELINA NGALULA ATEULIWA KUWA RAIS WA SHIRIKISHO LA SEKTA BINAFSI

 


Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) limetangaza uteuzi wa Rais na Makamu wa Rais wake wapya, kufuatia kuhitimishwa kwa mafanikio kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 24, uliofanyika tarehe 16 Oktoba 2026. 


Ampabo Bi. Angelina Ngalula ameteuliwa kuwa Rais wa Shirikisho hilo, Bi Ngalula ni mmiliki wa makampuni ya Bravo Group na Agricom.

Bw. Jitu Soni  ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais kwa akiwakilisha Tanzania Bara, Bw Soni ni Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania.

Bw. Ali Amour ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais akiwakilisha Zanzibar, Bw Amour ni Mwenyekiti wa wa Chemba ya Uchumi Zanzibar 


Uteuzi huu ni hatua muhimu katika kuimarisha uongozi, utawala, na mwelekeo wa kimkakati wa Shirikisho, huku likiendelea kutetea maslahi ya sekta binafsi nchini Tanzania. Kama chombo kikuu kinachowakilisha sekta binafsi nchini Tanzania.


TPSF ina jukumu muhimu katika kuratibu wadau wa sekta binafsi, kuimarisha majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, na kutetea mazingira wezeshi ya biashara yanayochochea uwekezaji, ukuaji wa biashara, ushindani, na maendeleo endelevu ya kiuchumi.

Hakuna maoni: