Breaking


Jumanne, 13 Oktoba 2026

MILIKI UBUNIFU MAJESHINI KULINDWA KISHERIA


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa, amezihimiza taasisi za majeshi nchini kusajili na kulinda bunifu zao kisheria ili kutambua umiliki wake, kuzuia matumizi yasiyoidhinishwa na kuongeza thamani ya bidhaa na huduma zinazozalishwa.


Bw. Nyaisa ameyasema hayo leo, wakati akifungua mafunzo kuhusu Miliki Ubunifu kwa Majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika mkoani Morogoro.


Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea maafisa wa majeshi uelewa kuhusu aina mbalimbali za miliki ubunifu zinazoweza kulindwa kisheria, zikiwemo alama za biashara na huduma (nembo), hataza za uvumbuzi, maumbo bunifu,  na nyenzo nyingine za miliki ubunifu.

Hakuna maoni: