Breaking


Jumatano, 28 Oktoba 2026

PROF. JANABI ATUNUKIWA TUZO YA JUU YA AFYA AFRIKA-DFAPH 2026



Abuja, Nigeria: Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika (WHO-AFRO), Mtanzania Profesa Mohamed Janabi, ametunukiwa tuzo ya heshima ya juu ya 'Distinguished Fellowship of the Academy of Public Health' (DFAPH 2026).


Tuzo hiyo imetolewa na The Pan-African Academy of Public Health Oktoba 25, 2026 jijini Abuja, ikiwatambua viongozi watano wa Afya barani Afrika wenye mchango mkubwa wa miongo kadhaa.


Kwa mujibu wa Academy, Profesa Janabi bingwa wa magonjwa ya Moyo, ametunukiwa kwa kazi yake ya kimfumo ya kuimarisha mitandao ya afya ya msingi barani Afrika na kukabiliana na changamoto za magonjwa yasiyoambukiza na magonjwa ya milipuko.


Baada ya kutunukiwa, Profesa Janabi ameandika ujumbe huu: "Naomba nichukue nafasi hii kwanza kuishukuru Serikali kuniamini. Wizara yetu ya Afya, Taasisi yetu ya JKCI, MNH, MOI na MUHAS na sekta na mahospitali yote nchini kwa imani na JKCI pamoja na hapa ninapo fanya kazi sasa WHO. Award hii ni kwa watanzania wote na niseme 'I am proud to be Tanzanian'. Ninajivunia kuwa Mtanzania (na pia mnyama sana) Asante wote."


Wengine waliotunukiwa tuzo hiyo pamoja na Prof. Janabi ni pamoja na: Profesa Mustapha Ferjani kutoka Tunisia, Profesa Nkandu Luo (Zambia), Profesa Awa Marie Coll Seck (Senegal) na Profesa Jean-Jacques Muyembe-Tamfum (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo).


Tuzo za DFAPH ni heshima ya juu zaidi ya Academy hiyo barani Afrika na hutolewa kila mwaka.


Hakuna maoni: