RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 mkoani Rukwa.
Maadhimisho hayo yatafanyika Oktoba 14, 2026 katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo katika Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, akizungumza katika kikao na wanahabari kilichofanyika mjini Sumbawanga leo ambacho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Vijana, Ajira na Uwekezaji Zanzibar, Ali Suleiman Ameir.
Alifafanua kuwa maadhimisho ya kilele hicho yanaenda sambamba na kuzimwa rasmi kwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambao uliwashwa Zanzibar Aprili 04 mwaka huu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi, dokta Husein Ali Mwinyi, ambapo umekumbizwa katika Halmashauri 195 zilizopo katika mikoa 31 Bara na Zanzibar.
Aidha maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru Kitaifa kitaendana na ibada takatifu ya kumbukizi ya miaka 27 ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere itakayofanyika katika kanisa Katoliki la mtakatifu Epifani saa 12:00 asubuhi mjini Sumbawanga.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni