Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, leo Oktoba 12, 2026, amepokea na kujadili taarifa ya Wizara pamoja na Taasisi zake kuhusu maandalizi ya kukabiliana na vipindi vya mvua kubwa vinavyotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Katika kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma, Waziri Kijaji amesisitiza umuhimu wa Wizara, Taasisi zake na Mamlaka za Hifadhi kujiandaa kikamilifu kuhakikisha miundombinu ya barabara katika hifadhi za taifa na vivutio vyote vya utalii nchini inaendelea kupitika wakati wote.
Amesema maandalizi hayo ni muhimu katika kuhakikisha mvua kubwa hazikwamishi shughuli za utalii, huku usalama wa watalii na mwendelezo wa huduma za utalii nchini ukipewa kipaumbele.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni