Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha usimamizi wa rasilimali watu, hususan ni maombi ya upandishaji na ubadilishaji vyeo kwa watumishi, kwa kusisitiza uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuhakikisha watumishi wanapata haki zao kwa wakati.
Akiongea leo Oktoba 21, 2026, katika ukumbi wa Wizara ya Afya, Mtumba jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Issa Ng’imba, amewataka watendaji kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na kuhakikisha maombi ya watumishi yanashughulikiwe kwa usahihi katika kila hatua.
“Niwaombe tuzingatie maelekezo yote na tujadili kwa kina maeneo yote ya kuzingatia ili kuhakikisha watumishi wanahudumiwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi,” amesema Bw. Ng’imba.
Kwa upande wake, Bi. Verediana V. Ngahega, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, amesisitiza umuhimu wa watendaji kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kutenda haki na kuongeza bidii ili kuwahudumia watumishi, hususan katika Sekta ya afya.
"Tufanye kazi kwa bidii ili kuweza kuwasaidia watumishi, hususan katika sekta hii ya afya,” amesema Bi. Ngahega.
Kikao kazi hicho kinalenga kuimarisha usimamizi wa maombi ya upandishaji na ubadilishaji vyeo kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa. Utekelezaji sahihi wa taratibu hizo ni muhimu katika kulinda haki za watumishi, kuimarisha uwajibikaji na kuongeza ari ya utendaji kazi katika Sekta ya Afya.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni