Wezi watu wazuri kabisa ameiba Hard Drives zenye muziki ambao haujatoka wa Beyoncé pamoja na vitu vingine kadhaa kutoka kwenye gari lililokodishwa na dancer wake wakati wa ziara ya Cowboy Carter huko Atlanta wiki iliyopita, kwa mujibu wa taarifa za polisi.
Kwa mujibu wa CNN, maafisa wa polisi walifika eneo la tukio Julai 8 baada ya kupokea simu ya taarifa ya wizi kutoka kwenye gari.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa masanduku mawili ya nguo yanayomilikiwa na choreographer Beyoncé, Christopher Grant, pamoja na mmoja wa dancers, Diandre Blue, yaliibwa kutoka kwenye gari la Jeep Wagoneer lililokuwa limeegeshwa ghorofa ya kwanza ya jengo la maegesho lililopo 99 Krog St. NE.
Kati ya vitu vilivyoibiwa ni laptop mbili na hard drive zilizokuwa na muziki wenye watermark, muziki ambao haujatolewa, mipango ya video, pamoja na orodha ya nyimbo za show zilizopita na zijazo.
Kitengo cha wizi kutoka kwenye magari cha Polisi wa Jiji la Atlanta kinachunguza tukio hilo. Polisi wamesema kibali cha kukamatwa kwa mtuhumiwa ambaye jina lake halijatajwa tayari kimetolewa.
Grant pia aliripoti kuibiwa nguo zenye thamani ya dola 1,000, miwani ya jua ya Tom Ford ya dola 500, na begi la mgongoni la Tumi la dola 750. Blue naye ameripoti kupoteza MacBook Air na headphones.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni