Breaking


Jumatatu, 28 Julai 2025

CCM YASISITIZA KUHESHIMU SHERIA ILI KUEPUSHA MACHAFUKO KATIKA UCHAGUZI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria na taratibu za uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki na wa amani, kikiahidi kukubali matokeo yoyote yatakayopatikana kwa mujibu wa taratibu halali.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis, ameyasema hayo Jiji Dar es Es salaam Wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa hakuna sababu ya kuwepo kwa machafuko iwapo sheria zitafuatwa kikamilifu na kila mdau wa uchaguzi ataheshimu taratibu zilizowekwa.

Amesisitiza kuwa ni wajibu wa vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi kuhakikisha kuwa sheria na taratibu za uchaguzi zinaheshimiwa ili kudumisha amani na utulivu wa taifa.

Khamis pia ameonya dhidi ya juhudi zozote za kuhujumu au kuingilia kazi ya Tume ya Uchaguzi, akisema kuwa hatua kama hizo zinaweza kuhatarisha uthabiti wa kisiasa na kijamii.

Kauli hiyo inakuja wakati taifa linapojiandaa na uchaguzi mkuu ujao, huku wito ukitolewa kwa wananchi na taasisi zote kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanabaki kuwa ya amani na heshima kwa mchakato wa kidemokrasia.

Hakuna maoni: