Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Emmanuel Nchimbi ametembelea Banda la NEMC Leo ikiwa ni siku ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoadhimishwa kila tarehe 05/06 ya Kila mwaka ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika kuhifadhi na kusimamia mazingira nchini.
Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika chini ya kaulimbiu isemayo *“Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania,”* ikihamasisha ushiriki wa wadau wote katika kutunza mazingira, kupambana na uharibifu wa mazingira na kuendeleza matumizi endelevu ya rasilimali asilia kwa maendeleo ya Taifa na ustawi wa vizazi vijavyo.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni