Kuelekea usiku wa tarehe 24 Julai 2026, mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini wanatarajiwa kushuhudia tamasha kubwa la ngumi litakalobeba jina la Dar Boxing Derby, tamasha ambalo linatajwa kurejesha hadhi ya ngumi za kweli tofauti na baadhi ya mapambano ambayo hivi karibuni yamekuwa yakilalamikiwa kuwa na drama nyingi zinazowachosha wapenzi wa mchezo huo.
Tamasha hilo linatarajiwa kukutanisha mabondia mbalimbali maarufu akiwemo Hussein Itaba, Dulla Mbabe, Juma Choki, Haidari Mchanjo pamoja na bondia wa ngumi za wanawake Sarah Alex ambaye ameendelea kujizolea umaarufu kutokana na uwezo wake mkubwa pamoja na mtindo wake wa kipekee wa kupigana.
Mbali na majina hayo, tamasha hilo pia litawakutanisha Debora Mwenda na mabondia wengine wenye ushindani mkubwa, hali inayozidi kuongeza hamasa kwa mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni