Breaking


Jumatatu, 28 Julai 2025

CIARA APATA URAIA WA BENIN, ASEMA “JE SUIS BÉNINOISE!” KWA FURAHA NA FAHARI! 🌍🎤🇧🇯


 Mwanamuziki maarufu duniani Ciara Princess Wilson ameandika historia mpyaya safari ya kutafuta mizizi yake imezaa matunda!  Tarehe 25 Julai 2025, Ciara aliwasili kwa mbwembwe kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cardinal Bernardin Gantin jijini Cotonou, Benin, na kupokewa kama malkia wa nyumbani! 

Akiwa amejaa hisia na furaha, Ciara alisimama mbele ya umati na kusema kwa lugha ya Kibenin, “Je suis Béninoise” (yaani “Mimi ni Mbenini”) tamko lililoamsha hisia kali kwa waliohudhuria na kufuatiwa na shangwe mitandaoni! 

Safari hii haikuwa tu ya kitalii bali ya kiroho na kihistoria. Ciara alichukua muda wake kuchunguza historia ya familia yake na kubaini kuwa ukoo wake mkubwa unatokea Benin. Uamuzi wake wa kuchukua uraia wa taifa hili la Afrika Magharibi ni wa kuvutia sana na umewagusa watu wengi duniani, hususan wale waishio ughaibuni ambao pia wana ndoto ya kugusa ardhi ya mababu zao. 

Katika picha na video zilizosambaa mitandaoni, Ciara anaonekana akiwa na tabasamu pevu, akiwa amevalia mavazi ya Kiafrika, akibembelezwa na ala za muziki wa jadi, huku wenyeji wa Benin wakimkaribisha kwa mapokezi ya kifalme. 

Watu wengi wamepongeza hatua hii kama mfano wa kuigwa, ishara ya kwamba ni muhimu kujua asili yako, kujivunia tamaduni zako na kuungana na historia ya familia yako. Wengine wamesema hatua ya Ciara ni mwamko mpya kwa waafrika wa diaspora kuungana tena na Bara lao la asili.

Kwa waliotaka kujua zaidi kuhusu nyota huyu, Ciara alizaliwa Oktoba 25, 1985 huko Austin, Texas, na maisha yake ya utotoni yalikuwa ya hapa na pale kutokana na kazi ya kijeshi ya baba yake, akihama kutoka Ujerumani hadi majimbo mbalimbali ya Marekani kabla ya familia yake kuhamia Atlanta, Georgia ambako ndoto yake ya muziki ilianza kuchanua.

Leo, Ciara si tu mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa duniani, bali pia ni Mbenini halisi mwenye moyo wa Kiafrika! 




#CiaraInBenin #JeSuisBeninoise #MiziziYaAfrika #FahariYaAsili #DiasporaToRoots




Hakuna maoni: