Katika tukio jingine la kisiasa lenye vionjo vya reality show, Rais wa Marekani, Donald Trump, ameamua kuvunja ukimya kwa kishindoakiwa kwenye ardhi ya Scotland! Safari hii, mshukiwa si mwingine bali ni Queen Bey mwenyewe —Beyoncé Knowles-Carter!
Trump amedai kwamba Beyoncé alipokea “malipo ya kimya kimya” ya zaidi ya dola milioni 11 ili kumuunga mkono Kamala Harris katika mkutano wa kampeni mwaka 2024 huko Houston. “Wamelipwa! Walivunja sheria! Washtakiwe!” alisikika akifoka kwenye mahojiano ya kisiasa yaliyojaa ushindani na shutuma zisizoisha.
Lakini hold up… kuna twist kubwa!
📉 Ukweli Unapiga Mzinga:
Kwa mujibu wa CNN, hakuna ushahidi hata wa centi moja kuthibitisha tuhuma hizo. Kumbukumbu rasmi zinaonyesha kwamba timu ya kampeni ya Kamala Harris ililipa kampuni ya utayarishaji ya Beyoncé dola 165,000 tu kwa gharama halali za maandalizi ya tukio hilo, si kwa endorsement au ushawishi wa kisiasa.
🤨 Uvumi Ulipotokea?
Taarifa za malipo hayo ya kutisha zilianza kutokota kwenye mitandao ya kijamii, zikichochewa na baadhi ya mashabiki sugu wa Trump mwaka 2024. Lakini tovuti za kuaminika kama FactCheck.org na PolitiFact zilisema hapana bana, hii ni propaganda tupu!
Mama mzazi wa Beyoncé, Tina Knowles, hakukaa kimya: “Binti yangu hakupokea hata senti! Alichofanya kilikuwa cha hiari na cha moyo mmoja.”
⚖️ Sheria Zinasemaje?
Wataalamu wa sheria wamebainisha kuwa hakuna sheria ya shirikisho inayokataza malipo kwa ajili ya ushiriki wa watu maarufu kwenye kampeni — ilimradi yapitie njia sahihi. Na hadi sasa? Hakuna malalamiko rasmi, wala ushahidi wa kufungua kesi dhidi ya Harris au Beyoncé.
🎬 Hitimisho la Filamu:
Ingawa madai ya Trump yanaonekana kama sinema ya siasa, ukweli bado unasimama imara kama nguzo. White House na timu ya Beyoncé wote wamekanusha vikali shutuma hizo.
Lakini kama kawaida, Donald Trump amethibitisha kuwa hapendi kupitwa na headlines, hasa ikiwa zinahusisha mastaa na wanasiasa wa chama pinzani!
Je, unadhani hii ni siasa au burudani? Tuambie kwenye maoni! 🗳️✨
📍 #MadelemoNews #TrumpVsBeyonce #Kamala2024 #PoliticalDrama



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni