Breaking


Alhamisi, 31 Julai 2025

MORICE ABRAHAM NI MNYAMA.


 Klabu ya Simba imemsajili kiungo Mtanzania, Morice Abraham kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Spartak Subotica ya Serbia.

Morice (21) alikuwa nahodha wa timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) iliyoshiriki mashindano ya AFCON mwaka 2019, yaliyofanyika Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba imesema kuwa baada ya mchezaji huyo kurejea nchini kutoka Serbia, alifanya mazoezi na timu ya Simba ambapo kocha Fadlu Davids pamoja na wasaidizi wake walivutiwa na uwezo wake, hivyo wakaamua kumsajili rasmi.


Hakuna maoni: