Breaking


Alhamisi, 31 Julai 2025

UWEPO WA KITUO CHA EACLC NI MATUNDA YA UBIA WA PPP-KAFULILA


Uzinduzi rasmi wa kituo cha Biashara cha East Africa Commercial and Logistics Center kilichopo Ubungo, kufanyika kesho.

Uzinduzi huo utafanywa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan, eneo la Ubungo jijini dar es salaam.

Kituo hicho kinatajwa kuwa hatua inayodhihirisha nia ya dhati ya Tanzania kujitambulisha kama taifa lenye nguvu ya kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kituo hiko kimeelezwa kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuwezesha upatikanaji wa ajira, kupunguza gharama za uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, na kuokoa muda uliokuwa ukitumika kwa wafanyabiashara kusafiri kwenda China na maeneo mengine duniani.

Nao, baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Kariakoo, akiwemo Husna Suleiman na Rajabu Musa, wameeleza matumaini yao kuwa kituo hicho cha ubungo kitasaidia zaidi kupunguza gharama za usafiri na kuongeza unafuu wa bei za bidhaa kwa watumiaji wa mwisho.

Kufuatia hali hiyo Dira Kuu ya Habari ya Uhuru FM imezungumza na mtaalamu wa masuala ya Fedha na Uchumi, Damian Edward, ambaye amesema uwepo wa kituo hicho ni hatua madhubuti katika kuinua uchumi wa taifa. 

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi-PPPC, David Kafulila, amesisitiza kuwa sekta binafsi zina mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa nchi na uwekezaji, na uwepo wa kituo hicho cha Ubungo cha EACLC ni matunda ya ubia wa PPP.

Kufunguliwa kwa kituo cha biashara cha East Africa Commercial and Logistics Center kunatajwa kuwa mojawapo ya miradi mikubwa ya kimkakati inayoendelea kuibadilisha Tanzania kuwa kitovu cha biashara kimataifa.

Hakuna maoni: