Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC, limeitunuku Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania-Tantrade, Tuzo ya utunzaji bora wa mazingira wakati wa maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba.
Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Khamis, amepokea Tuzo hiyo kwa niaba ya taasisi hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dokta Immaculate Sware Semesi, katika hafla ya kufunga maonesho hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imetolewa kutambua juhudi za Tantrade katika kuhakikisha usafi, udhibiti wa taka na matumizi ya mbinu rafiki kwa mazingira katika eneo la maonesho pamoja na kuwa na siku maalumu ya mazingira wakati wa maonesho.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni