Kumekuwa na ongezeko la Asilimia 194 kwenye mauzo ya bidhaa mbalimbali wakati wa maonesho ya mwaka huu ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania-TanTrade, Latifa Khamis, amesema mwaka uliopita mauzo yalifikia zaidi ya shilingi Bilioni-300 na mwaka huu ni zaidi ya shilingi Bilioni-700.
Kupitia maonesho hayo, wafanyabiashara wamepata fursa za bidhaa mbalimbali zenye thamani ya shilingi Bilioni-400 katika kipindi cha maonesho ya 49 pekee, huku asilimia 70 ya wafanyabisha walioshiriki maonesho hayo wakitimiza malengo yao.
Kwa mujibu wa Latifa, TanTrade inajipanga kuwa na maonesho ya kipekee mwaka 2026, ambapo maonesho hayo yatakuwa yanatimiza miaka 50 tangu yalipoanza mwaka 1976.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni