Mtangazaji wa kituo cha radio Mjini Fm Perfect Crispin
ameomba radha kwa kilichotokea kati yake na msanii Dogo Patten, Ameandika kupitia akaunti yake ya instagramu👇🏽👇🏽
TAARIFA KWA UMMA
Kumradhi.
Ningependa kuchukua fursa hii kuwaomba radhi za dhati kabisa kwa mwenendo nilioonyesha mbele ya mgeni wetu, mdogo wangu, msanii Dogo Paten siku ya tarehe 07/17/25 katika kipindi cha Radio cha Gen Tok ambako mimi ni mmoja wa Presenters wake.
Kitendo kile cha kumshambulia kwa maneno na kumtaka ajibu maswali kwa lazima si cha hadhi,sio cha kitaaluma na ni kitendo cha utovu wa nidhamu sio tu kwa mgeni wetu lakini pia kwenu wasikilizaji wetu.
Tukio lile limenifedhehesha mimi binafsi, familia yangu hali kadhalika wote ambao mliotegemea ubora wangu katika kazi hii kama mlivyonizoea na kwa kweli hamkustahili.
Ninakiri kuchafua taswira yangu binafsi, yenu waskikizaji na ya kituo changu cha kazi.Naomba mniwie radhi.
Nalichukua suala hili kwa uzito mkubwa kwanza kwa kukiri kuwa nimekosea na halikuwa kusudio langu lakini pili, kumuomba tena msamaha wa dhati mdogo wangu, msanii Dogo Paten kwa tabia niliyoionyesha kwake. Hakika haikuwa sawa na sio hulka yangu! kama binadamu nina mapungufu na hili sikudhamiria na ni la kibinaadamu na niwaahidi kuwa linarekebishika.
Namshukuru sana Mdogo wangu, msanii Dogo Paten, walezi wangu kitaaluma Bodi ya Ithibati kwa mwongozo mzuri na malezi na naahaidi kufuata maagizo yote mliyonipatia ili nijifunze zaidi na zaidi katika taaluma hii niipendayo sana.Mimi bado mwanafunzi na daima nitabaki hivyo.
Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wote mliotoa maoni yenu katika suala hili na ninahaidi kwa roho safi kupokea maoni hayo kama sehemu ya kujifunza zaidi na yote mliyosema nitayazingatia Bila kinyongo.
Nashukuru sana kwa kusoma ujumbe wangu huu na barua hii ya samahani yangu kwenu nyote niliowakwaza huku nikiomba muwe tayari kunipokea tena ili tuendeleze uhusiano mzuri tuliojenga kwa miaka mingi kwa pamoja nami nikibaki tayari kujifunza.
Hii ni Video baada ya kufunga show na kwenda na kumuweka sawa..Hii ni kuwaonesha love nakumuelewesha Situation nzima.. 🫶🏾
Ndimi mtiifu!
Perfect Crispin.
@dogo.paten @basata.tanzania @tcra_tanzania @wizara_sanaatz @mwanafa @prof.kabudipjam

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni