Bosi wa Manchester United, Ruben Amorim, anataka kusajii wachezaji wawili zaidi katika dirisha hili la usajili (Mirror).
United pia wamepeleka ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Sporting Viktor Gyokeres, 27, na wanatumai wanaweza kumshawishi ajiunge nao na kuiacha Arsenal (A Bola).
Na walikataliwa nia yao ya kumsajili mshambuliaji wa Italia Francesco Pio Esposito, 20, na Inter Milan mnamo Januari (Football Italia).
Mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, amekamilisha vipimo vyake vya afya kwa Manchester United, na hivyo kutua Old Trafford kutoka Brentford (Fabrizio Romano).

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni