Timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars, imejiondoa katika michuano ya CECAFA Four Nations yanayoanza Julai 21 jijini Arusha.
Uamuzi huo umefikiwa kufuatia ushauri wa benchi la ufundi la timu, baada ya kufanya tathmini ya maandalizi na mazingira yaliyopo, ambayo yalionekana kuwa hayafai kwa ushiriki wa timu.
Mashindano hayo yalitarajiwa kuzikutanisha timu za taifa za Tanzania (wenyeji), Uganda, Kenya na Senegal.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni