Breaking


Jumamosi, 26 Julai 2025

WAPIGA KURA 37,655,559 WAMEJIANDIKISHA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU 2025


 TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema wapigakura 37,655,559 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu 2025.

Kati ya hao wapiga kura wapya ni 7,641,592 sawa na asilimia 136.79 ya makadirio ya awali.

Idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 26.55 kutoka milioni 29.7 waliokuwa wamejiandikisha katika daftari mwaka 2020.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji (Rufaa) Jacob Mwambegele amesema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa ratiba ya uchaguzi huo jijini Dodoma.

Hakuna maoni: