TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC),imezindua ratiba ya uchaguzi Mkuu 2025,inayoonyesha tarehe ya kupiga kura kuwa ni Octoba 29,2025.
Pia,Agosti 28 hadi Octoba 28 ni Kampeni za uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara na Agosti 28 hadi Octoba 27 mwaka huu ni Kampeni za uchaguzi Tanzania Zanzibar ili kupisha kura za mapema.
Akizindua ratiba hiyo leo Jijini Dodoma mbele ya waandishi wa habari na wadau kutoka vyama vya siasa 18,Mwenyekiti wa INEC Jaji(Rufaa)Jacob Mwambegele amesema Agosti 9 hadi 27 mwaka huu ni zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi kwa ajili ya wagombea wa Urais na Makamu wa Rais.
Aidha,Agosti 14 hadi 27,2025,ni utoaji wa fomu za uteuzi wa waliogombea nafasi ya ubunge na udiwani na uteuzi wa wagombea Urais,Makamu wa Rais,Wabunge na Madiwani ni Agosti 27 mwaka huu.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni