Breaking

Jumatatu, 4 Agosti 2025

MAN UNITED WAKO TAYARI KUTOA OFA SAWA NA NEWCASTLE KUMNYAKUA BENJAMIN SESKO WA RB LEIPZIG

 

Manchester United wako tayari kutoa ofa ya kwanza inayofanana na Newcastle kwa ajili ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia, Benjamin Sesko, 22. (Sky Sports Germany)

Newcastle pia wanataka kumchukua mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ureno, Goncalo Ramos, 24, ikiwa mpango wa Sesko utashindikana. (Daily Mail)

 Inter Milan wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Uingereza, Mason Greenwood, 23, kutoka klabu ya Ufaransa ya Marseille. (Corriere Dello Sport - in Italian)

Klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig iliulizia kuhusu winga wa Uingereza, Tyrique George, 19, wakati wa mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa kiungo kutoka Uholanzi, Xavi Simons, 22. (Fabrizio Romano)


Hakuna maoni: