Breaking


Jumanne, 12 Agosti 2025

MGOMBEA URAIS AFARIKI DUNIA COLOMBIA



Mgombea urais wa Colombia, Miguel Uribe, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo ikiwa ni miezi miwili tangu aliposhambuliwa alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi.

Licha ya dalili zilizoleta matumaini katika wiki za hivi karibuni, madaktari walitangaza kuwa mwanasiasa huyo alianza kuvuja damu kwenye Ubongo Jumamosi iliyopita.

Juni 7, 2025, Uribe, aliyekuwa Seneta wa kihafidhina mwenye umri wa miaka 39, alipigwa risasi kichwani na mguuni alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji Mkuu Bogota.

Watuhumiwa sita wanaohusishwa na shambulio hilo wamekamatwa, akiwemo mshambuliaji anayetajwa kuwa kijana mwenye umri wa miaka 15. 

Kifo cha mgombea huyo ambaye angelichuana na Rais Gustavo Petro katika uchaguzi wa mwakani, kimezusha hofu ya kuiona Colombia ikirejea katika ghasia za kisiasa.

Hakuna maoni: