Breaking


Jumamosi, 6 Septemba 2025

MAKAMBAKO KWA NYOMI HILI MMETUHESHIMISHA- RAIS SAMIA

MGOMBEA Urais kupitia Chama ChaMapinduzi(CCM),Rais Dkt.Samia Suluhu,amelakiwa  na mamia ya wakazi wa Makambako na kupata nafasi ya kunadi sera na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030.

Akizungumza na wananchi hao Septemba 6,2025,Rais Samia amewashukuru kwa kujitokeza kwa wingi licha ya kwamba mkutano huo ulikuwa ni wa njiani na ni asubuhi.

"Ndugu zangu wana Makambako nawashukuru sana,kwa umma huu ni ishara kuwa mmeturidhia nasi tunasema ahsante sana,"amesema.

Amesema ameenda kwa mambo mawili kueleza waliyoyafanya na wanayoyatarajia kuyafanya baadae ili Octoba 29,2025,wakapige kura kwa CCM.

Hakuna maoni: