Breaking


Jumamosi, 6 Septemba 2025

FUTURE NA CIARA: MTOTO WAO FUTURE JR. AONGEZEWA JINA “WILSON” KISHERIA, MASHABIKI WAZUA MJADALA


 Mtoto wa msanii maarufu wa muziki Future na na mpenzi wake wa zamani Ciara, anayejulikana kwa jina la Future Jr., sasa rasmi ameongezewa jina “Wilson” kisheria. 

Hata hivyo, bado anabaki na jina la ukoo la baba yake mzazi, Wilburn. Kwa mujibu wa taarifa kutoka TMZ, mabadiliko haya yalifanyika miaka michache iliyopita.


Wiki hii, mjadala ulizuka mitandaoni baada ya Russell Wilson, mume wa Ciara, kuposti picha akimuita kijana huyo kwa jina “Future Wilson.” Tukio hilo lilipelekea mashabiki wengi kuamini kuwa huenda Wilson amemlea rasmi kama mwanawe wa kisheria.


Hata hivyo, taarifa rasmi zinaonyesha kuwa jambo hilo ni mabadiliko ya majina pekee na si uthibitisho wa ulezi wa kisheria kama baadhi ya mashabiki walivyodhani.




Chanzo: TMZ


Hakuna maoni: