Breaking


Jumamosi, 6 Septemba 2025

TUTAFANYA UTAFITI KUONGEZA MAENEO YA UCHIMBAJI MADINI- DOKTA NCHIMBI

 

Mgombea Mwenza Kupitia Chama Cha Mapinduzi Balozi Dokta Emmanuel Nchimbi amesema katika kipindi cha miaka mitano Serikali ya CCM imefanya 

maendeleo mengi ikiwemo utoaji leseni kwa wachimbaji wa mbogwe ambapo mpaka sasa Jumla ya Leseni 41 zimetolewa. 

Aidha Dokta Nchimbi amesema kwa Serikali inaendelea kufanya utafiti wa kuangalia upatikanaji wa madibi Wilayani Mbogwe kutokana na wananchi wengi kupenda kujishughulisha na uchimbaji. 

Dokta Nchimbi amesema hayo Septemba 05, 2025 kwenye Mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Wilayani mbogwe mkoani Geita. 

Pia Dokta Nchimbi amesema pamoja na kufanya tafiti lakini Serikali ya CCM itatenga maeneo ya maalum ya wachimbaji wadogo sababu wao ndio wanakwenda kutengeneza wachimbaji wakubwa wanakuwa matajiri ambao wanachangia miradi ya maendeleo na kodi kwa maendeleo ya nchi. 

Pia amesema kwenye eneo la madini iwapo CCM itashinda watakwenda kutenga maeneo ya maalum ya wachimbaji wadogo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bukombe Dokta Dotto Biteko amewataka wananchi wa Mbogwe kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku itakapofika.

Hakuna maoni: