Breaking

Ijumaa, 24 Oktoba 2025

MKUU WA MKOA WA ARUSHA CPA. AMOS MAKALLA AKUBALI KUWA MLEZI WA TIMU YA MBUNI FC, ATOA MILIONI 13.5 KUCHOCHEA SAFARI YA LIGI KUU


 MKUU wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA. Amos Gabriel Makalla, rasmi amekubali kuwa Mlezi wa Timu ya mpira wa Miguu ya Mbuni FC yenye Makao yake Makuu Mkoani humo, kufuatia ombi lililowasilishwa kwake na JWTZ Brigedi ya Kanda ya Kaskazini.

CPA. Makalla ameanza ulezi huo rasmi  Oktoba 23,2025, alipokutana na kuzungumza na Menejimenti na Wachezaji wa timu hiyo na kutoa shilingi milioni 13.5 kwa ajili ya posho na motisha kwa wachezaji huku akiwataka kuanza safari ya kuipandisha timu hiyo ili kucheza Ligi kuu, kama sehemu ya kukuza utalii wa Michezo Arusha.



Hakuna maoni: