Mwanamuziki staa wa Afrika Kusini Tyla, ambaye ametikisa dunia kupitia hit zake kama Water, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto alizopitia katika safari ya kujitambua kama mtu wa jamii ya coloured kundi la watu wenye asili mchanganyiko nchini humo 🇿🇦.
Akiwa anasaka ndoto zake shuleni, Tyla anakiri alipitia kipindi kigumu. Anasema alipokuwa shule ya msingi, ambapo wanafunzi wengi walikuwa weupe, mara nyingi alijihisi hafai na hana ujasiri. 😔
“Nilihisi kama sipo sehemu sahihi, sikujua ni upande gani ninafaa kuwa,” alisema kwa uchungu.
Lakini mambo yalibadilika alipohamia shule ya sekondari yenye wanafunzi wengi weusi. Hapo ndipo Tyla alianza kujipenda zaidi, kujiona mrembo, na kujijengea kujiamini. 💃
“Nilianza kuelewa uzuri wangu wa kipekee, na kwamba sina haja ya kujilinganisha na mtu mwingine,” aliweka wazi.
Katika mahojiano yake na jarida la Glamour, Tyla alisisitiza kuwa uzoefu huo ulimfundisha somo kubwa maishani kwamba kuwa coloured si udhaifu, bali ni nguvu na urithi wa kipekee wa Afrika Kusini. 🌍✨
Kwa sasa, Tyla anasema anaishi maisha ya kujivunia alipotoka na kutambua thamani yake kama msanii na kama mwanamke wa Kiafrika. ❤️🇿🇦





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni