Breaking


Jumatatu, 6 Oktoba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU: CHELSEA SASA YAMTAKA MSHAMBULIAJI WA BOURNEMOUTH ANTOINE SEMENYO

 

Chelsea imesitisha mpango wa kumsajili beki wa Crystal Palace Marc Guehi, 25, licha ya beki huyo wa Uingereza kupatikana kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Express)

Chelsea, hata hivyo, ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo na iko tayari kulipa takriban £78m kumpata mshambuliaji huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 25. (Fichajes - kwa Kihispania)

Beki wa zamani wa Tottenham na Manchester United Sergio Reguilon yuko kwenye mazungumzo kuhusu uhamisho wa kushtukiza ili kuungana na Lionel Messi katika klabu ya Ligi Kuu ya Soka (MLS) Inter Miami baada ya mkataba wake na Spurs kumalizika majira ya kiangazi. (Mail)


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: