Breaking

Ijumaa, 14 Novemba 2025

CAMARA WA SIMBA SC KUFANYIWA UPASUAJI MOROCCO

 

Mlinda mlango wa Simba SC, Moussa Camara, anatarajiwa kuondoka nchini kesho kuelekea Morocco kwa ajili ya matibabu maalum na upasuaji wa goti unaotarajiwa kufanyika Jumatatu, Novemba 17.


Camara alipata majeraha hayo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, mchezo ambao ulilazimika kumtoa uwanjani kutokana na maumivu makali ya goti.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, kipa huyo atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 8 hadi 10, kipindi ambacho kitapangwa kulingana na hatua za matibabu na mwitikio wa mwili wake wakati wa kurejea kwenye programu za mazoezi.


Simba SC inatarajia kurejea kwake kwa nguvu mpya baada ya kukamilisha hatua zote za tiba, huku nafasi yake golini ikiachwa mikononi mwa makipa wengine wa kikosi hicho wakati wa kipindi cha mpito.


Hakuna maoni: