Timu ya Menejimenti ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) imefuatilia kwa umakini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyotolewa leo Novemba 14, 2025, wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13 jijini Dodoma.
Timu ya Menejimenti ya TVLA ilikusanyika katika ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya TVLA yaliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam, ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa TVLA, Dkt. Stella Bitanyi. Baada ya hotuba hiyo, viongozi hao walipata fursa ya kujadili kwa pamoja masuala muhimu yaliyogusiwa na Rais, hususan maboresho ya sekta ya mifugo, uzalishaji na usambazaji wa chanjo za mifugo, pamoja na umuhimu wa uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Menejimenti ilisisitiza kuwa maelekezo ya Rais yatakuwa dira muhimu katika kuimarisha mipango na utekelezaji wa majukumu ya TVLA kwa kipindi kijacho. Aidha, uongozi huo umeonesha utayari wa kuongeza ubunifu, ufanisi na ushirikiano na wadau ili kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya sekta ya mifugo na uchumi wa Taifa.
TVLA imedhamiria kuendelea kushiriki kikamilifu katika ajenda za Serikali kwa kutoa huduma za maabara zenye viwango, kuimarisha usalama wa chakula, na kulinda afya ya mifugo pamoja na wananchi.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni