Breaking

Ijumaa, 14 Novemba 2025

CARDI B AJIFUNGUA MTOTO WA NNE NA MPENZI WAKE MPYA STEFON DIGGS


 Rapper maarufu wa Marekani, Cardi B, amejifungua mtoto wake wa nne, ambaye pia ni mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake mpya, nyota wa NFL Stefon Diggs.

Taarifa kutoka timu yake imethibitisha kuwa mama na mtoto wote wako salama, ingawa bado haijawekwa wazi jinsia ya mtoto huyo.

Baada ya kutangaza habari hizo njema, Cardi B aliandika ujumbe wa hisia kupitia ukurasa wake wa Instagram, akieleza shukrani na hatua mpya katika maisha yake:

“Maisha yangu yamekuwa mchanganyiko wa sura na misimu tofauti. Kuanza upya si rahisi, lakini imekuwa ya thamani! Nimeleta muziki mpya, albamu mpya, na sasa mtoto mpya duniani.”

Katika video aliyochapisha, Cardi anaonekana akiimba wimbo wake Hello, huku akieleza namna mtoto huyo mpya alivyoleta mwanga na motisha katika maisha yake:

“Mtoto huyu amenipa sababu nyingine ya kuwa toleo bora zaidi la mimi mwenyewe kunipenda zaidi ili niwape watoto wangu upendo na maisha wanayostahili. Hii sura mpya ni Mimi dhidi ya Mimi mimi dhidi ya kila kizuizi kinachonizuia.”

Aidha, aliweka wazi kuwa anaendelea kujiandaa kwa ziara yake mpya ya kimataifa, huku akitoa kipaumbele kwenye afya yake ya mwili na akili.

“Hakuna kitakachonizuia kuwapa mashabiki wangu onesho la maisha yao. Nimejifunza, nimepona, na ninampenda mwanamke niliyekuwa sasa.”

Kwa ujio huu mpya, Cardi B sasa ni mama wa watoto wanne. Watatu wa kwanza  Kulture, Wave, na Blossom aliwapata akiwa na rapa Offset.

Hakuna maoni: