Magari 50 yameanza kutoa huduma ya usafirishaji wa muda katika Barabara ya Morogoro kufuatia kusitishwa kwa mabasi yaendayo haraka (UDART), hatua inayolenga kupunguza adha ya usafiri iliyokumba wakazi wa Kimara, Mbezi na Kibaha.
Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Dar es Salaam, Pateli Ngereza Tengeneza, amesema kuwa mamlaka imetoa leseni za muda kwa magari 50 kati ya 150 yaliyopangwa kutoa huduma hiyo, jambo litakalosaidia kupunguza msongamano wa abiria hasa nyakati za asubuhi na jioni.
Ngereza amebainisha kuwa vibali hivi ni vya muda na vinawawezesha wamiliki wa magari kutoa huduma katika njia kuu kama Mbezi-Mnazi Mmoja, Makumbusho na Posta. Wamiliki waliokuwa na leseni za awali hawatapoteza vibali vyao, kwani baada ya kipindi cha muda kuisha, watarejea katika njia zao za awali bila gharama yoyote ya ziada.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni