Bilionea kutoka Afrika Kusini, Patrice Motsepe, ameendelea kupanua himaya yake ya uchimbaji madini baada ya kununua mgodi mkubwa wa shaba uliopo nchini Australia.
Motsepe, ambaye ni mwanzilishi wa kampuni ya African Rainbow Minerals (ARM), amesaini mkataba wa manunuzi wa mgodi huo wenye thamani ya dola bilioni 1.
Kampuni hiyo ni miongoni mwa makampuni makubwa zaidi barani Afrika yanayojihusisha na uchimbaji wa madini mbalimbali kama dhahabu, shaba, chuma na makaa ya mawe.
Hatua hii inaashiria kuongezeka kwa ushawishi wa Motsepe katika sekta ya madini duniani, huku ikisisitiza dhamira yake ya kuwekeza katika rasilimali zenye thamani ya juu katika maeneo mbalimbali duniani.
“Lengo langu ni kuona kampuni zetu kutoka Afrika zikishindana na kuongoza katika uchimbaji na biashara ya madini duniani kote,”
Patrice Motsepe

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni