Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa maeneo mbalimbali nchini, kama ifuatavyo,
Mikoa ya Kigoma, Kagera na Geita: Mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache.
Tanga, Mtwara, Unguja na Pemba: Mawingu kiasi na mvua katika maeneo machache.
Dar es Salaam na Pwani (pamoja na Mafia): Mawingu kiasi na mvua nyepesi katika maeneo machache.
Ruvuma na Lindi: Mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Morogoro, Singida na Dodoma, pamoja na Manyara, Arusha na Kilimanjaro, na Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya, pamoja na Tabora, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara: Mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Upepo wa pwani: Unavuta km 20 kwa saa; bahari mawimbi madogo.
Matarajio ya Alhamisi: Mabadiliko madogo ya hali ya hewa.
Utabiri umetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni