Hapa tunakuletea utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo, ili uwe na mpango mzuri wa siku yako. Taarifa hii imetolewa na TMA, kuanzia saa 3.00 usiku wa leo.
Hali ya Hewa Kwenye Mikoa Mbalimbali:
- Mkoa wa Kagera: Mawingu kiasi, vipindi vya jua.
- Visiwa vya Unguja na Pemba: Mawingu kiasi na jua likiangaza mara kwa mara.
- Mikoa ya Dar es Salaam na Tanga: Jua kali na mawingu kidogo.
- Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora: Mawingu kiasi, vipindi vya jua.
- Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi: Hali ya jua kali, mawingu kidogo.
- Mikoa ya Morogoro, Singida na Dodoma: Mawingu kiasi, vipindi vya jua.
- Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro: Mawingu kiasi na jua mara kwa mara.
- Mkoa wa Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia): Jua kali, mawingu kidogo.
- Mikoa ya Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya: Mawingu kiasi, vipindi vya jua.
- Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara: Mawingu kiasi, jua likiangaza mara kwa mara.
Kwa ujumla, hali ya hewa leo inatarajiwa kuwa ya mawingu kiasi na vipindi vya jua katika sehemu nyingi za nchi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni