Imefahamika kuwa kujiondoa kwa kundi la waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka mji muhimu wa Uvira kumetokana na agizo la Marekani.
Inaelezwa kuwa Marekani iliapa kulichukulia hatua kundi hilo kutokana na uvunjaji wa wazi wa mkataba wa amani uliosimamiwa na Ikulu ya White House.
Kundi hilo linaloungwa mkono na Rwanda lilichukua udhibiti wa mji huo wa kimkakati karibu na mpaka wa Burundi wiki iliyopita, siku chache baada ya serikali za Congo na Rwanda kusaidi mkataba wa amani mjini Washington, mkataba ambao Rais Donald Trump aliusifia.
Hatua hiyo ya M23 imeutia doa mchakato huo wa amani na kuzusha hofu za vita vikubwa zaidi vya kikanda.
Kwa kuushikilia kwake mji wa Uvira uliliwezesha kundi hilo kudhibiti mpaka wa Congo na Burundi na kuikatia serikali mjini Kinshasa msaada wa kijeshi kutoka jirani yake huyo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni