Breaking


Jumapili, 14 Desemba 2025

MEZA YA MAGAZETI LEO | JUMAPILI, DESEMBA 14, 2025

 


Karibu katika Meza ya Magazeti ya leo, ambapo tunakuletea muhtasari wa vichwa vikuu vilivyojitokeza katika magazeti ya Jumapili, Desemba 14, 2025. Magazeti yameangazia kwa kina masuala ya michezo, afya, siasa na kijamii yanayoendelea kutikisa jamii.


Gazeti la MwanaSpoti limeipa uzito habari za michezo likiandika kwa herufi kubwa kuhusu hatima ya kocha wa Simba SC, likieleza sababu zinazomuweka kocha Zambeba katika wakati mgumu. Pia, limeangazia maisha ya mastaa wa burudani pamoja na taarifa za Ligi Kuu ya England.

Kwa upande wake, Nipashe Jumapili limeibua mjadala mzito wa kiafya kupitia kichwa cha habari kinachohusu ongezeko la visa vya ngiri kwa wanaume, sambamba na tahadhari kwa jamii. Gazeti hilo pia limeandika kuhusu ratiba ya mgao wa maji iliyotolewa na DAWASA, pamoja na habari za kijamii na kitaifa.










Endelea kufuatilia blog yetu kwa uchambuzi mpana wa kila kichwa cha habari pamoja na undani wa matukio muhimu yanayoikumba Tanzania na dunia kwa ujumla.


Hakuna maoni: