Serikali Yaahidi Kuimarisha Ushirikiano na NDC Kukuza Viwanda, Ajira na Uchumi wa Taifa Naibu Waziri wa Viwanda na biashara Patrobas Katambi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo Tanzania (NDC) katika kuendelea kukuza biashara na uchumi.
Katambi ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika ofisi za NDC zilizopo Posta Dar es Salaam.
Aidha amesema anaipongeza NDC, kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana na watu wa makamo kama njia ya kuendelea kuthamini maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu kuwekeza na kuwajali vijana.
Amesema NDC imeendelea kukuza uchumi wa nchi kwa kufufua Viwanda vilivyopo nchini, huku akisema wao kama wizara wataendelea kufufua Viwanda zaidi ili kukuza ajira kwa vijana.
Kwa upande mwingine Katambi, amesema ili kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 NDC kwa kushirikiana na Serikali wanahitaji kukuza uchumi wenye tija kwa Wananchi na vijana ambao ndilo taifa la keeshond.
Pia amesema yupo kwa ajili ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kama kuna mtu mwenye mawazo chanya na ya kujenga basi asisite kumuuliza muda wowote na yeye kama mshauri wa Waziri basi atayafikisha maoni hayo ili kujenga msingi bora wa biashara na kukuza uchumi wa nchi.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni