Breaking


Jumamosi, 27 Desemba 2025

TANESCO YATOA TAARIFA KWA UMMA KUHUSU CHANGAMOTO YA MANUNUZI YA UMEME (LUKU)

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kumetokea changamoto ya manunuzi ya umeme (LUKU) hali inayosababisha wateja kushindwa kununua umeme kupitia njia za mitandao ya simu, na njia za kibenki.


Tayari Watalaamu wetu kwa kushirikiana na wataalamu wa GePG wanashughulikia changamoto iliyojitokeza ili huduma iweze kurejea katika hali ya kawaida.


Tunawashauri wateja wetu kununua umeme kupitia vituo vya mawakala wetu wa

LUKU nchi nzima.


Shirika litawafahamisha wateja wake huduma zitakaporejea kikamilifu.


Hakuna maoni: