Breaking


Jumamosi, 27 Desemba 2025

TRA YADHIMINI LIGI YA MKOA WA KAGERA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera jana tarehe 26 Desemba 2025, katika Uwanja wa Kaitaba, Manispaa ya Bukoba, imedhamini mashindano ya Ligi ya Mkoa wa Kagera kwa kutoa mahitaji mbalimbali kwa timu shiriki.

Mahitaji hayo yamejumuisha fedha taslimu kwa ajili ya uendeshaji, jezi kwa timu zote shiriki, pamoja na zawadi mbalimbali kwa washindi, pamoja na kombe kwa timu mshindi wa mashindano hayo.

Hafla ya ufunguzi wa ligi hiyo ilipambwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya timu ya Leo Tena na Greenland, uliovutia mashabiki wengi wa soka kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera.

Vifaa hivyo  vilikabidhiwa rasmi na Meneja wa TRA Mkoa wa Kagera, Bw. Castro John, ambaye pia alitumia fursa hiyo kutoa elimu ya kodi kwa wananchi na wadau wa michezo waliohudhuria. Aidha, alieleza namna ambavyo TRA inavyoshirikiana na walipa kodi katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ikiwemo kuunga mkono michezo kama chombo cha mshikamano na maendeleo ya vijana.


TRA Mkoa wa Kagera imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kushirikiana na jamii katika kuchochea maendeleo kupitia michezo na ulipaji kodi kwa hiari.

Hakuna maoni: