Mkuu wa Mkoa Morogoro Mhe. Adam Malima ameikabidhi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tuzo kwa kudhamini mashindano ya michezo yanayoratibiwa na Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Kampuni binafsi (SHIMMUTA) yaliyofanyika Morogoro kuanzia tarehe 25.11.2025 kumaliza tarehe 06.12.2025.
Tuzo hiyo ilipokelewa na katibu wa timu ya michezo ya TRA, Bw. Kamna Shomari kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda tarehe 6.12.2025 mjini Morogoro.
Katika mashindano hayo TRA iliweza kupokea tuzo za ushindi mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza kwa upande wa mpira wa miguu.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni