Breaking


Ijumaa, 6 Februari 2026

HAWA HAPA MAKATIBU WAKUU WAWILI WA WIZARA YA NISHATI

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya muundo wa Wizara ya Nishati Kwa kuwa na Makatibu Wakuu wawili ambapo mmoja atashughulikia masuala ya mafuta na gesi na mwengine atakayeshughulikia masuala ya umeme na mafuta jadidifu.

Katika taarifa iliyotolewa leo Februari 06, na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt Moses Kusiluka, Rais Dkt Samia pia amemteua Dkt James Peter Mataragio kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, anayeshughulikia mafuta na gesi asilia na Mhandishi Felchesmi Jossen Mramba ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshugulikia masuala ya umeme na nishati jadidifu.

Hakuna maoni: