Breaking


Jumamosi, 7 Februari 2026

JUX NA PRISCILLA WAADHIMISHA MWAKA MMOJA WA NDOA KWA HISIA ZA KIFILAMU

 


Msanii Jux na mkewe Priscilla Ajoke (Priscy) wameadhimisha mwaka mmoja tangu wafunge ndoa yao kwa mtindo wa kipekee uliojaa sanaa, mapenzi na kumbukumbu za kihistoria za filamu. Kupitia ujumbe wao mfupi lakini wenye uzito, “One year down & forever to go”, wanandoa hao wameweka wazi kuwa safari yao ya ndoa ni simulizi inayoendelea iliyofungwa kwa ubunifu na upendo wa dhati.


Kilichowavutia wengi ni namna Priscy alivyochagua kuwasilisha maadhimisho hayo kupitia picha alizochapisha kwenye Instagram, zikiwa zimebuniwa kwa msukumo wa filamu maarufu Poetic Justice ya mwaka 1993. Filamu hiyo iliyochezwa na mastaa Janet Jackson na Tupac Shakur imeacha alama kubwa katika historia ya sanaa na mapenzi, na sasa imepewa uhai mpya kupitia picha za kisasa zenye ladha ya nostalgia.

Kuanzia mavazi yaliyopangwa kwa ustadi, mitindo ya kupiga pose, hadi hisia (mood) ya picha, kila undani umeakisi uhalisia wa Poetic Justice. Mchanganyiko huu wa filamu ya kihistoria na simulizi ya ndoa ya kisasa umeifanya sherehe yao ya mwaka mmoja kuwa zaidi ya maadhimisho bali kuwa kazi ya sanaa inayosimulia mapenzi kwa lugha ya picha.

Kwa mtindo huu, Jux na Priscy wameonesha kuwa mapenzi yanaweza kuadhimishwa kwa ubunifu unaovuka mipaka ya kawaida, na kuacha kumbukumbu itakayodumu milele.

Hakuna maoni: