Jana, Jennifer Lopez alionekana hadharani akiwa na mwanae, lakini kilichovutia na kushangaza wengi siyo tu kuonekana kwao pamoja, bali mtindo na muonekano wa mwanae, ambao haujazoeweka kwa macho ya mashabiki wengi. Picha na video zao zilisambaa kwa kasi, huku baadhi ya watu wakianza kuibua maswali kuhusu afya na hali ya mtoto huyo.
Hata hivyo, Jennifer Lopez amevunja ukimya na kuweka mambo wazi, akisisitiza kuwa mwanae yuko salama kabisa kiafya na hana tatizo lolote. Kwa mujibu wa JLo, mabadiliko yanayoonekana kwa sasa yanahusiana na kupenda mitindo (fashion) na kujitambulisha kimtindo kama vijana wengine wa kizazi cha sasa.
Kauli hiyo ya Jennifer Lopez imepokelewa kwa hisia mseto, huku wengine wakimpongeza kwa kumuunga mkono mwanae, na wengine wakisisitiza umuhimu wa jamii kuheshimu maamuzi binafsi, hasa kwa watoto wa watu maarufu.
Kwa sasa, gumzo linaendelea kutawala mitandao ya kijamii, likionyesha namna maisha ya watu maarufu yanavyoendelea kuwa chini ya uangalizi mkubwa wa umma.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni